23 Mei 2025 - 18:58
Sheikh Abdul Ghani | "Kila hatua katika Maisha ya Mwislamu inapaswa kuzingatia lengo kuu, na Lengo kuu sio njaa wala mkate"

Uuzaji wa Heshima kwa Mabepari: Sheikh alilaani wazi wale wanaoisaliti Palestina na kuipendelea dunia kwa kubadilisha heshima yao kwa manufaa ya watawala dhalimu.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA - Ufuatao ni Muhtasari wa Hotuba ya Ijumaa ya leo nchini Kenya iliyotolewa na Samahat Sheikh Abdul Ghani Khatibu. Hotuba hiyo ilibeba ujumbe mzito na wa msingi kwa Umma wa Kiislamu, hasa katika nyanja za uongozi, thamani ya utu wa Mwanadamu, na msimamo wa Kiislamu kuhusu dhulma na mabepari (watawala waovu).

Sheikh Abdul Ghani | "Kila hatua katika Maisha ya Mwislamu inapaswa kuzingatia lengo kuu, na Lengo kuu sio njaa wala mkate"

Katika ujumbe huu, tunaona:

  1. Umuhimu wa Malengo Safi: Sheikh alisisitiza kuwa kila hatua katika maisha ya Mwislamu inapaswa kuzingatia lengo kuu – kuhifadhi utu, hadhi, na heshima ya kibinadamu.

  2. Hatari ya Kuchagua Viongozi kwa Maslahi ya Kifedha: Mfano wa “bei ya mkate” ulitumika kwa ufasaha kuonyesha kuwa kuchagua viongozi kwa misingi ya maslahi ya muda mfupi husababisha udhalilishaji wa jamii.

    Sheikh Abdul Ghani | "Kila hatua katika Maisha ya Mwislamu inapaswa kuzingatia lengo kuu, na Lengo kuu sio njaa wala mkate"

  3. Uuzaji wa Heshima kwa Mabepari: Sheikh alilaani wazi wale wanaoisaliti Palestina na Wapalestina na kuipendelea dunia kwa kubadilisha Hadhi na Heshima yao kwa manufaa ya watawala dhalimu.

    Sheikh Abdul Ghani | "Kila hatua katika Maisha ya Mwislamu inapaswa kuzingatia lengo kuu, na Lengo kuu sio njaa wala mkate"

  4. Mwito wa Mageuzi Chanya: Mwisho, aliwasihi Waislamu warejee katika misingi ya Mwenyezi Mungu ili kuishi kwa Hadhi na Heshima kama wanadamu waliotukuka, na kama alivyowaumba Mwenyezi Mungu, kwa sababu Mwenyezi Mungu amemtukuza Mwanadamu na amempa Hadhi na Heshima kubwa katika viumbe Vyake. Mwanadamu anatakiwa kuishi Heshima hii na Hadhi hii na kamwe asiuze Heshima yake kwa thamani yoyote ile.

    Sheikh Abdul Ghani | "Kila hatua katika Maisha ya Mwislamu inapaswa kuzingatia lengo kuu, na Lengo kuu sio njaa wala mkate"

    Sheikh Abdul Ghani | "Kila hatua katika Maisha ya Mwislamu inapaswa kuzingatia lengo kuu, na Lengo kuu sio njaa wala mkate"

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha